Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia majirani
Yakobo 2 : 8
8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.
Marko 12 : 31
31 ⑪ Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Mithali 3 : 29
29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
Mithali 25 : 17 – 18
17 Mguu wako usiingie katika nyumba ya jirani yako ila kwa kiasi; Asije akakukinai na kukuchukia.
18 ⑯ Mtu amshuhudiaye jirani yake uongo Ni nyundo, na upanga, na mshale mkali.
Warumi 15 : 2
2 Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.
Wagalatia 5 : 14
14 ⑩ Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Mathayo 7 : 12
12 ⑰ Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.
Luka 6 : 31
31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
Warumi 13 : 10
10 ⑤ Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.
Mambo ya Walawi 19 : 16 – 18
16 ⑳ Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu[9] ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.
17 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, au ulipizwe uovu kwa ajili yake
18 Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA.
Zekaria 8 : 17
17 ③ wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.
Warumi 12 : 19
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Luka 10 : 27
27 ① Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
Kutoka 20 : 16
16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
Mathayo 19 : 19
19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
Zekaria 8 : 16
16 ② Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme ukweli na jirani yake; katika malango yenu toeni hukumu za kweli na ziletazo amani;
Zaburi 15 : 1 – 3
1 BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayeishi Katika kilima chako kitakatifu?
2 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake,
3 Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala kumtenda mwenziwe mabaya, Wala kumsengenya jirani yake.
Leave a Reply