Biblia inasema nini kuhusu majira ya joto โ€“ Mistari yote ya Biblia kuhusu majira ya joto

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia majira ya joto

Zaburi 74 : 17
17 Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia, Majira ya joto na ya baridi wewe uliyafanya.

Luka 21 : 30
30 Wakati imalizapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.

Amosi 8 : 1
1 Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, kikapu cha matunda ya wakati wa joto.

Zaburi 32 : 4
4 Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.

Yeremia 8 : 20
20 Mavuno yamepita, wakati wa joto umekwisha, wala sisi hatukuokoka.

Mithali 26 : 1
1 Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.

Marko 13 : 28
28 Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu;

Yakobo 1 : 17
17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.

Mwanzo 8 : 22
22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.

Mithali 6 : 6 โ€“ 8
6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

Luka 21 : 29 โ€“ 36
29 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote.
30 Wakati imalizapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.
32 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita kabla ya hayo yote kutimia.
33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
34 Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 โ‘  Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.

Mathayo 24 : 32
32 Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu;

Mithali 10 : 5
5 Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *