Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Maji
Zaburi 148 : 5
5 Na vilisifu jina la BWANA, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.
Mwanzo 1 : 9
9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
Ezekieli 4 : 11
11 Nawe utakunywa maji kwa kuyapima, sehemu ya sita ya hini; utayanywa kwa wakati wake.
2 Wafalme 20 : 20
20 ⑯ Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na ushujaa wake wote, tena alivyolifanya birika na mfereji, akaleta maji ndani ya mji, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?
Ezekieli 47 : 5
5 Kisha akapima dhiraa elfu moja, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika.
Hesabu 19 : 22
22 ⑮ Na kitu chochote atakachokigusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi; na mtu atakayekigusa kitu hicho atakuwa najisi hadi jioni.
Kutoka 17 : 1
1 ⑰ Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.
Kutoka 17 : 6
6 Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.
Hesabu 20 : 11
11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.
Waamuzi 15 : 19
19 ⑥ Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore,[14] napo pa katika Lehi hata hivi leo.
2 Wafalme 3 : 20
20 ⑱ Ikawa asubuhi, wakati wa kutoa sadaka ya unga, tazama, maji yakaja kwa njia ya Edomu, hata nchi ikajaa maji.
2 Wafalme 2 : 22
22 Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.
Kutoka 14 : 22
22 ⑭ Wana wa Israeli wakaenda ndani wakipita kwenye nchi kavu ndani ya bahari; huku maji yakiwa ukuta kwao mkono wa kulia na mkono wa kushoto.
Yoshua 3 : 17
17 ⑱ Na hao makuhani waliolichukua sanduku la Agano la BWANA wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hadi taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.
2 Wafalme 2 : 8
8 Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu.
Leave a Reply