Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Majeraha, Matibabu ya
Mithali 20 : 30
30 Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikia ndani ya mtima.
Isaya 1 : 6
6 Toka wayo wa mguu hadi kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwazongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.
Luka 10 : 34
34 akakaribia, akamfunga majeraha yake, akayatia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
Leave a Reply