Biblia inasema nini kuhusu majaribu na dhiki – Mistari yote ya Biblia kuhusu majaribu na dhiki

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia majaribu na dhiki

1 Petro 5 : 10
10 Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.

Yakobo 1 : 12
12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Warumi 12 : 12
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;

Kutoka 14 : 14
14 ⑦ BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

Mithali 3 : 5 – 6
5 ③ Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6 ④ Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

Waraka kwa Waebrania 10 : 35
35 Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.

1 Wakorintho 10 : 13
13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.

Yohana 16 : 33
33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Wafilipi 4 : 6 – 7
6 Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Zaburi 23 : 4
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

Warumi 5 : 3
3 ⑰ Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta subira;

Yakobo 1 : 2 – 8
2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
5 Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.

Warumi 8 : 18
18 Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.

Yakobo 1 : 2
2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;

Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

1 Petro 4 : 12
12 ④ Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.

Warumi 8 : 28
28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Yoshua 1 : 9
9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

Mathayo 19 : 26
26 Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *