Biblia inasema nini kuhusu Mafuta – Mistari yote ya Biblia kuhusu Mafuta

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mafuta

Kutoka 23 : 18
18 Usinitolee damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hadi asubuhi.

Kutoka 29 : 13
13 ① Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.

Kutoka 29 : 22
22 Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo dume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kulia; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu;

Mambo ya Walawi 1 : 8
8 kisha wana wa Haruni, makuhani, watazipanga kuni zilizo juu ya moto uliopo juu ya madhabahu;

Mambo ya Walawi 3 : 5
5 Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.

Mambo ya Walawi 3 : 11
11 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Mambo ya Walawi 3 : 16
16 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.

Mambo ya Walawi 4 : 10
10 vile vile kama yanavyoondolewa katika ng’ombe wa kuchinjwa kwa sadaka za amani; kisha huyo kuhani atayateketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.

Mambo ya Walawi 7 : 5
5 ⑩ na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kuwa dhabihu kwa BWANA kwa njia ya moto; ni sadaka ya hatia.

Mambo ya Walawi 8 : 16
16 Kisha akayatwaa mafuta yote yaliyokuwa katika matumbo yake, na kitambi kilichokuwa katika ini, na figo zake mbili, na mafuta yake, na Musa akayateketeza juu ya madhabahu.

Mambo ya Walawi 8 : 26
26 ④ kisha kutoka kwa kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichokuwa pale mbele za BWANA, akatwaa mkate mmoja usiochachwa, na mkate mmoja ulioandaliwa na mafuta na kaki moja nyembamba, akaiweka juu ya mafuta, na juu ya huo mguu wa nyuma wa upande wa kulia;

Mambo ya Walawi 10 : 15
15 Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama BWANA alivyoagiza.

Mambo ya Walawi 17 : 6
6 Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za BWANA.

1 Samweli 2 : 16
16 Tena, ikiwa mtu yule amwambia, Hawakosi wataichoma moto hayo mafuta kwanza, kisha utwae kadiri roho yako itakavyopenda; ndipo husema, Sivyo, lakini sharti unipe sasa hivi; la, hunipi, basi nitaitwaa kwa nguvu.

Isaya 43 : 24
24 Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako.

Mambo ya Walawi 3 : 16
16 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.

Mambo ya Walawi 3 : 17
17 Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.

Mambo ya Walawi 7 : 23
23 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yoyote, ya ng’ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi.

Kumbukumbu la Torati 32 : 38
38 Uliokula shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia ninyi; Na wawe hao himaya yenu.

Mwanzo 45 : 18
18 ⑲ kisha mkamtwae baba yenu, na watu wa nyumbani mwenu, mkanijie; nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.

Mwanzo 49 : 20
20 Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme.

Zaburi 37 : 20
20 Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.

Zaburi 81 : 16
16 Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.

Isaya 25 : 6
6 ⑲ Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *