Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mafundisho ya uongo
1 Yohana 4 : 1
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
2 Wakorintho 11 : 13 – 15
13 ⑲ Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
Waefeso 6 : 10 – 18
10 ⑥ Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 ⑦ Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 ⑧ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 ⑩ Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 ⑪ Basi simameni, mkiwa mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 ⑫ na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani;
16 ⑬ zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 ⑭ Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 ⑮ kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Leave a Reply