Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mafundisho
Yohana 7 : 17
17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
Matendo 15 : 29
29 yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
Mathayo 5 : 19
19 ⑩ Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Mathayo 15 : 9
9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Mathayo 15 : 13
13 Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.
Warumi 16 : 18
18 ⑪ Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.
1 Wakorintho 3 : 11
11 ⑳ Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
1 Wakorintho 3 : 21
21 Basi, mtu yeyote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu;
1 Wakorintho 3 : 4
4 ⑮ Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?
1 Wakorintho 11 : 19
19 ⑬ kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.
2 Wakorintho 2 : 17
17 ① Kwa maana sisi si kama walio wengi, walichuuzao neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.
2 Wakorintho 11 : 4
4 ⑫ Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au Injili nyingine msiyoikubali, mnavumiliana naye punde!
Wagalatia 1 : 8
8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi Injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe.
Waefeso 4 : 14
14 ② ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Wakolosai 2 : 4
4 ⑤ Nasema neno hili, mtu asije akawadanganya kwa maneno ya kuwashawishi.
Wakolosai 2 : 8
8 ⑩ Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
Wakolosai 2 : 23
23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
1 Timotheo 1 : 4
4 wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na kikomo, zinazozua maswali wala si mpango[1] wa Mungu ulio katika imani; basi uwaambie hivyo.
1 Timotheo 1 : 7
7 wakitaka kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.
1 Timotheo 1 : 19
19 uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia katika Imani.
1 Timotheo 4 : 3
3 ⑬ wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
1 Timotheo 4 : 7
7 ⑮ Bali hadithi za kale, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.
1 Timotheo 6 : 5
5 na kuzozana miongoni mwa watu waliopotoka katika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
1 Timotheo 6 : 21
21 ④ ambayo wengine kwa kuikiri wamepoteza Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.
2 Timotheo 2 : 14
14 Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wanaoyasikia.
2 Timotheo 2 : 18
18 waliopotoka kutoka kwenye kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha tokea, hata kuipindua imani ya watu kadhaa.
Leave a Reply