Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mafanikio
Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Zaburi 37 : 4
4 Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.
Mathayo 6 : 25 – 33
25 ④ Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?⑤
26 ⑥ Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 ⑦ nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 ⑧ Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 ⑩ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Mithali 3 : 1 – 4
1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.
2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
3 ① Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 ② Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
Yakobo 4 : 10
10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Mithali 16 : 3
3 Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli.
1 Wafalme 2 : 3
3 ④ uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;
Mathayo 16 : 26
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Luka 16 : 10 – 11
10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na asiyeaminika katika lililo dogo, huwa haaminiki pia katika lililo kubwa.
11 Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya duniani, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli?
Zaburi 1 : 1 – 6
1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
6 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.
Mithali 3 : 3 – 4
3 ① Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 ② Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
Yoshua 1 : 5 – 9
5 Hakuna mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.
6 Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
7 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.
Yoshua 1 : 8
8 Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Mithali 3 : 5
5 ③ Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Wagalatia 5 : 22 – 23
22 ⑮ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 ⑯ upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Isaya 41 : 10
10 ② usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Kumbukumbu la Torati 8 : 18
18 ⑳ Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
Mwanzo 39 : 2 – 6
2 BWANA akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.
3 Bwana wake akaona ya kwamba BWANA yu pamoja naye, na ya kuwa BWANA anafanikisha mambo yote mkononi mwake.
4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
5 Ikawa tokea wakati alipomweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Baraka za BWANA zikawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu chochote chake, ila hicho chakula alichokula tu. Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri.
Leave a Reply