Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mabua
Kutoka 15 : 7
7 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokupinga, Huwatumia hasira yako nayo huwateketeza kama mabua makavu.
Ayubu 21 : 18
18 Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba?
Zaburi 83 : 13
13 Ee Mungu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, Kama ya makapi mbele ya upepo,
Isaya 5 : 24
24 Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.
Isaya 40 : 24
24 Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.
Isaya 41 : 2
2 Ni nani aliyemwinua mmoja atokaye mashariki, ambaye katika haki amemwita mguuni pake? Ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme; awatoa wawe kama mavumbi kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake.
Isaya 47 : 14
14 ⑦ Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa kutoka kwa nguvu za muali wa moto; hili halitakuwa kaa la kujipasha moto, wala moto wa kuota.
Yeremia 13 : 24
24 Kwa sababu hiyo nitawatawanya, kama makapi yapitayo, kwa upepo wa jangwani.
Yoeli 2 : 5
5 Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto iunguzapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita.
Nahumu 1 : 10
10 Kwa maana kama miiba wametatana, kama walevi wamelewa, watateketezwa kama mabua makavu.
Malaki 4 : 1
1 Kwa maana,[1] angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Leave a Reply