Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Luka
Wakolosai 4 : 14
14 ⑬ Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.
Luka 1 : 4
4 upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa.
Matendo 1 : 2
2 hadi siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua;
Matendo 16 : 13
13 Siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.
Matendo 20 : 6
6 Sisi tukatweka baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filipi, tukawafikia Troa, baada ya safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.
Matendo 21 : 18
18 Hata kesho yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako.
2 Timotheo 4 : 11
11 Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi.
Filemoni 1 : 24
24 na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami.
Leave a Reply