Biblia inasema nini kuhusu Libna – Mistari yote ya Biblia kuhusu Libna

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Libna

Hesabu 33 : 20
20 Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapiga kambi Libna.

Yoshua 10 : 32
32 BWANA akautia huo mji wa Lakishi mkononi mwa Israeli, naye akautwaa siku ya pili, akaupiga kwa makali ya upanga, na wote pia waliokuwamo ndani yake, sawasawa na hayo yote aliyoutenda Libna.

Yoshua 10 : 39
39 kisha akautwaa, na mfalme wake, na miji yake yote; nao wakawapiga kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa wote pia waliokuwamo ndani yake; hakumwacha hata mmoja aliyesalia; kama alivyoufanyia Hebroni aliufanyia na Debiri vivyo hivyo, na mfalme wake; kama alivyoufanyia Libna, na mfalme wake.

Yoshua 12 : 15
15 mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;

Yoshua 21 : 13
13 Kisha wakawapa wana wa Haruni, kuhani, Hebroni pamoja na mbuga zake za malisho yake, huo mji wa kukimbilia kwa ajili ya mwuaji, na Libna pamoja na malisho yake;

1 Mambo ya Nyakati 6 : 57
57 Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake;

2 Wafalme 19 : 8
8 Basi yule kamanda akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru, anapigana na Libna; maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi.

2 Wafalme 19 : 35
35 ① Ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia moja themanini na tano elfu. Na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.

Isaya 37 : 36
36 ⑪ Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *