Biblia inasema nini kuhusu Lango la Samaki โ€“ Mistari yote ya Biblia kuhusu Lango la Samaki

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Lango la Samaki

2 Mambo ya Nyakati 33 : 14
14 Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya Lango la Sameki; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka makamanda wa jeshi katika miji yote ya Yuda yenye maboma.

Nehemia 3 : 3
3 Na lango la samaki wakalijenga wana wa Senaa; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.

Sefania 1 : 10
10 Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *