Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Labani
Mwanzo 28 : 5
5 Basi Isaka akamtuma Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.
Mwanzo 22 : 23
23 Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Abrahamu.
Mwanzo 24 : 15
15 ⑳ Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Abrahamu, naye ana mtungi begani pake.
Mwanzo 24 : 29
29 Na Rebeka alikuwa na kaka, jina lake Labani. Labani akatoka mbio kumwendea yule mtu kisimani.
Mwanzo 24 : 33
33 Akaandaliwa chakula, lakini akasema, Sili mpaka niseme kwanza maneno yangu. Akamwambia, Haya, sema.
Mwanzo 29 : 30
30 Ndipo Yakobo[14] akaingia kwa Raheli, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine.
Mwanzo 29 : 20
20 Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda.
Mwanzo 29 : 27
27 timiza siku zake saba, nasi tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine.
Mwanzo 30 : 43
43 ⑩ Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.
Mwanzo 30 : 43
43 ⑩ Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.
Mwanzo 31 : 21
21 Basi akakimbia yeye na yote aliyokuwa nayo; akaondoka akauvuka mto, na kuelekea kwenye nchi ya milima ya Gileadi.
Mwanzo 31 : 55
55 Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao.
Leave a Reply