Biblia inasema nini kuhusu kwaya โ€“ Mistari yote ya Biblia kuhusu kwaya

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kwaya

2 Mambo ya Nyakati 5 : 12 โ€“ 14
12 tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, wakiwa wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia moja na ishirini wakipiga panda;)
13 hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA,
14 hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa BWANA.

Wakolosai 3 : 16
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

1 Wakorintho 14 : 26
26 โ‘ฃ Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

Nehemia 12 : 31 โ€“ 43
31 โ‘ฑ Ndipo nikawapandisha viongozi wa Yuda juu ya ukuta, nikawatenga makundi mawili makubwa ya hao walioandamana na kushukuru, liende upande wa kulia ukutani kuliendea lango la jaa;
32 na baada yao wakaenda Hoshaya, na nusu ya wakuu wa Yuda,
33 na Azaria, na Ezra, na Meshulamu,
34 na Yuda, na Benyamini, na Shemaya, na Yeremia,
35 โ‘ฒ na baadhi ya makuhani wenye baragumu; Zekaria, mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu;
36 โ‘ณ na ndugu zake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda, na Hanani, wenye vinanda vya Daudi mtu wa Mungu; Ezra, mwandishi, akawatangulia;
37 na kwa lango la chemchemi, wakienda moja kwa moja mbele yao, wakapanda madaraja ya mji wa Daudi, uinukapo ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, mpaka lango la maji upande wa mashariki.
38 Na kundi la pili wao wenye kushukuru wakaenda kuwalaki, na mimi nikafuata nyuma yao, pamoja na nusu ya watu, ukutani juu ya mnara wa tanuri, mpaka ule ukuta mpana;
39 na juu ya lango la Efraimu, na kupita lango la kale, na lango la samaki, na mnara wa Hananeli, na mnara wa Hamea, mpaka lango la kondoo; nao wakasimama hapo langoni pa gereza.
40 Ndivyo walivyosimama makundi mawili yao walioshukuru nyumbani mwa Mungu, na mimi, na nusu ya viongozi pamoja nami;
41 na makuhani, Eliakimu, Maaseya, Miyamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania, wenye baragumu;
42 na Maaseya, na Shemaya, na Eleazari, na Uzi, na Yehohanani, na Malkiya, na Elamu, na Ezeri. Waimbaji wakaimba kwa sauti kuu, akiwa Yezrahia msimamizi wao.
43 Wakatoa dhabihu nyingi siku ile, wakafurahi; kwa kuwa Mungu amewafurahisha furaha kuu; na wanawake pia na watoto wakafurahi; hata ikasikika mbali sana furaha hiyo ya Yerusalemu.

Yakobo 5 : 13
13 Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.

Zaburi 100 : 1 โ€“ 5
1 Mshangilieni BWANA, enyi nchi zote;
2 Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake mkiimba;
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 Maana BWANA ni mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake katika vizazi vyote.

Ayubu 38 : 7
7 โ‘  Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

1 Wakorintho 14 : 40
40 โ‘ง Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *