Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kwaya
Zaburi 105 : 1 – 45
1 Haleluya.[16] Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake.
2 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Yasimulieni maajabu yake yote.
3 Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
4 Mtafuteni BWANA na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote.
5 Yakumbukeni matendo yake ya ajabu aliyoyafanya, Miujiza yake na hukumu alizotoa.
6 Enyi wazawa wa Abrahamu, mtumishi wake; Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7 Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Hukumu zake ziko duniani kote.
8 Analikumbuka agano lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
9 Agano alilofanya na Abrahamu, Na ahadi yake kwa Isaka.
10 Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, Na Israeli liwe agano la milele.
11 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Kama fungu la urithi wenu.
12 Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa, Naam, watu wachache na wageni katika nchi,
13 Wakatangatanga toka taifa hadi taifa, Toka ufalme mmoja hadi kwa watu wengine.
14 Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao.
15 Akisema, Msiwaguse masihi[17] wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.
16 ① Akasababisha njaa katika nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
17 ② Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani.
18 ③ Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma.
19 Hadi wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya BWANA ilimjaribu.
20 ④ Mfalme alituma watu na kumfungua, Mkuu wa watu akamwachilia huru.
21 ⑤ Akamweka kuwa mkuu wa nyumba yake, Na mwenye mamlaka juu ya mali yake yote.
22 Awaongoze maofisa wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima.
23 ⑥ Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.
24 ⑦ Akawajalia watu wake wazae sana, Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.
25 Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake.
26 ⑧ Akamtuma Musa, mtumishi wake, Na Haruni ambaye amemchagua.
27 Akatenda mambo ya ishara zake kati yao, Na miujiza katika nchi ya Hamu.
28 ⑩ Alituma giza, na kufanya nchi kuwa na giza, Wakayaasi maneno yake.
29 ⑪ Aliyageuza maji yao yakawa damu, Akawaua samaki wao.
30 ⑫ Nchi yao ilijaa vyura, Hata nyumbani mwa wafalme wao.
31 ⑬ Alisema, kukaja makundi ya mainzi, Na chawa katika nchi yao yote.
32 ⑭ Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe, Na umeme uliomulika ghafla katika nchi yao.
33 Akaipiga mizabibu yao na mitini yao, Akaivunja miti ya nchi yao.
34 ⑮ Alisema, kukaja nzige, Na tunutu wasiohesabika;
35 Wakaila miche yote ya nchi yao, Wakayala matunda ya ardhi yao.
36 ⑯ Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi, Malimbuko ya nguvu zao.
37 ⑰ Akawatoa wakiwa na fedha na dhahabu, Katika makabila yao asiwepo mwenye kujikwaa.
38 Misri ilifurahi walipoondoka, Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.
39 ⑱ Alitandaza wingu liwe kifuniko, Na moto ili uwaangazie usiku.
40 ⑲ Walimwomba naye akaleta kware, Na kuwashibisha chakula cha mbinguni.
41 ⑳ Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita jangwani kama mto.
42 Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Abrahamu, mtumishi wake.
43 Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.
44 Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu;
45 Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya.
Mithali 16 : 3
3 Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli.
2 Timotheo 2 : 15
15 Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.
Wafilipi 4 : 8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Leave a Reply