Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuzaliwa katika dhambi
Zaburi 51 : 5
5 ③ Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia; Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi.
Warumi 5 : 12
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Zaburi 58 : 3
3 ③ Waovu hupotoka hata kabla ya kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
Mhubiri 7 : 20
20 ⑦ Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, atendaye mema pasipo kutenda dhambi.
Warumi 3 : 23
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Warumi 5 : 19
19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.
Mwanzo 8 : 21
21 BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 1
1 Yohana 1 : 10
10 Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, tunamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo ndani yetu.
Mithali 22 : 15
15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Ayubu 15 : 14 – 16
14 ⑦ Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
15 ⑧ Yeye hawategemei watakatifu wake; Naam, mbingu nazo si safi machoni pake.
16 ⑩ Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu, Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!
Ezekieli 28 : 15
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
Yeremia 17 : 9
9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Yakobo 4 : 17
17 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.
Leave a Reply