Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuweka nyuma nyuma
Wafilipi 3 : 13 – 14
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
14 nakaza mwendo, niifikie tuzo la thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
2 Wakorintho 5 : 17
17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.
Wagalatia 2 : 20
20 ① Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Wafilipi 3 : 13
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
2 Wakorintho 5 : 17 – 18
17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.
18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.
Wafilipi 3 : 14
14 nakaza mwendo, niifikie tuzo la thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Yohana 5 : 16 – 18
16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
17 ① Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
18 ② Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
Yohana 3 : 3
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Isaya 24 : 1 – 23
1 Tazama, BWANA ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.
2 ④ Na itakuwa kama ilivyo hali ya watu, ndivyo itakavyokuwa hali ya kuhani; kama ilivyo hali ya mtumwa, ndivyo itakavyokuwa hali ya bwana wake; kama ilivyo hali ya mjakazi, ndivyo itakavyokuwa hali ya bibi yake; kama ilivyo hali yake anunuaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake auzaye; kama ilivyo hali yake akopeshaye, ndivyo itakavyokuwa hali yake akopaye; kama ilivyo hali yake atwaaye faida, ndivyo itakavyokuwa hali yake ampaye faida.
3 Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana BWANA amenena neno hilo.
4 Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.
5 ⑤ Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.
6 ⑥ Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia, ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea, watu waliosalia wakawa wachache tu.
7 Divai mpya inaomboleza, mzabibu umedhoofika, watu wote waliochangamka moyo wanaugua.
8 Sauti ya furaha ya matoazi inakoma; kelele yao wafurahio imekwisha; furaha ya kinubi inakoma.
9 Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; kileo kitakuwa uchungu kwao wakinywao.
10 Mji wa machafuko umebomolewa; kila nyumba imefungwa, asipate kuingia mtu awaye yote.
11 Pana kilio katika njia kuu kwa sababu ya divai; furaha yote imetiwa giza, na changamko la nchi limetoweka.
12 Ndani ya mji umebaki ukiwa, na lango lake limepigwa kwa uharibifu.
13 Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake.
14 Hawa watainua sauti zao, watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa BWANA watapiga kelele toka baharini.
15 ⑦ Basi, mtukuzeni BWANA katika mashariki, litukuzeni jina la BWANA, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.
16 ⑧ Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.
17 ⑩ Hofu, na shimo, na mtego, viko juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.
18 ⑪ Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika.
19 ⑫ Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.
20 Dunia inalewalewa kama mlevi, nayo inawayawaya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.
21 ⑬ Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia;
22 nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi wataadhibiwa.
23 ⑭ Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Yohana 21 : 15 – 25
15 ⑯ Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda[6] kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
16 ⑰ Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo wangu.
17 ⑱ Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
18 ⑲ Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.
19 ⑳ Akasema neno hilo kwa kuonesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.
20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)
21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?
22 Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe? Wewe unifuate mimi.
23 Basi neno hilo lilienea katikati ya ndugu ya kwamba mwanafunzi yule hafi. Lakini Yesu hakumwambia ya kwamba hafi; bali, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe?
24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
25 Pia kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
Warumi 12 : 3
3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
Zaburi 37 : 1 – 40
1 Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, Usiwahusudu wafanyao ubatili.
2 Maana kama majani watakatika mara, Kama miche mibichi watanyauka.
3 Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
4 Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.
5 Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumainie, naye atakutendea.
6 Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.
7 Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
9 Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali, Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.
10 Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
11 Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.
12 Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake.
13 BWANA atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.
14 Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta, Wamwangushe chini maskini na mhitaji, Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.
15 Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe, Na nyuta zao zitavunjika.
16 Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
17 Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
18 BWANA huwatunza waaminifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.
19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.
20 Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
21 Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22 Maana waliobarikiwa na BWANA watairithi nchi, Nao waliolaaniwa naye watakatiliwa mbali.
23 Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA, Naye huipenda njia yake.
24 Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
25 Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.
26 Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.
27 Jiepushe na uovu, utende mema, Na kukaa hata milele.
28 Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
29 Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.
30 Kinywa chake mwenye haki hunena hekima, Na ulimi wake husema hukumu.
31 Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake. Hatua zake hazitelezi.
32 Mtu asiye haki humvizia mwenye haki, Na kutafuta jinsi ya kumwua.
33 BWANA hatamwacha mkononi mwake, Wala hatamwacha alaumiwe atakapohukumiwa.
34 Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
35 Nimemwona mtu asiye haki mkali sana, Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.
36 Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana.
37 Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
38 Wakosaji wataangamizwa pamoja, Wasio haki mwisho wao wataharibiwa.
39 Na wokovu wa wenye haki una BWANA; Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
40 Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; Huwaopoa kutoka kwa wasio haki na kuwaponya; Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.
Warumi 6 : 1 – 6
1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?
3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;
Leave a Reply