Biblia inasema nini kuhusu kuwatia nidhamu watoto – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuwatia nidhamu watoto

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuwatia nidhamu watoto

Waefeso 6 : 4
4 ② Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.

Waraka kwa Waebrania 12 : 11
11 ⑳ Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoeshwa nayo matunda ya haki yenye amani.

Mithali 19 : 18
18 Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.

Mithali 23 : 13 – 14
13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.

Mithali 29 : 17
17 ⑫ Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako.

Waefeso 6 : 2 – 3
2 ① Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.

Mithali 29 : 15
15 Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *