Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuwasiliana na wafu
Kumbukumbu la Torati 18 : 10 – 12
10 ⑫ Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 ⑬ wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 ⑭ Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
Mambo ya Walawi 20 : 27
27 ⑭ Tena mwanamume au mwanamke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.
Isaya 8 : 19
19 ③ Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
Mambo ya Walawi 19 : 31
31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
1 Yohana 4 : 1
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
2 Wakorintho 11 : 14
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Zaburi 6 : 5
5 ⑤ Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
1 Timotheo 4 : 1
1 ⑫ Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
Zaburi 146 : 4
4 ⑰ Pumzi yake inapomtoka, anarudi katika udongo wake, Siku iyo hiyo mipango yake hutoweka.
Mhubiri 9 : 5
5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana tuzo tena; maana hata kumbukumbu lao limesahauliwa.
Zaburi 115 : 17
17 Wafu hawamsifu Mungu BWANA, Wala yeyote ashukaye kwenye kimya;
Leave a Reply