Biblia inasema nini kuhusu kuwaadhibu watoto wako – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuwaadhibu watoto wako

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuwaadhibu watoto wako

Mithali 23 : 13 – 14
13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.

Mithali 22 : 15
15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

Kumbukumbu la Torati 21 : 18 – 21
18 ⑫ Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi,
19 ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake;
20 wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi.
21 ⑬ Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.

Mithali 22 : 6
6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Mithali 29 : 15
15 Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.

Waefeso 6 : 4
4 ② Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.

Waraka kwa Waebrania 12 : 6 – 7
6 ⑰ Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humuonya Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
7 Ni kwa ajili ya kuonywa mnastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyeonywa na babaye?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *