Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuvuka mipaka
Isaya 55 : 8 – 9
8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
Isaya 40 : 22
22 Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
Ayubu 11 : 6 – 7
6 ⑯ Tena akuoneshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako.
7 ⑰ Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikia upeo wa huyo Mwenyezi?
Ayubu 26 : 7
7 ⑯ Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
2 Petro 2 : 4
4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Leave a Reply