Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kutoroka
Mwanzo 3 : 11
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Mwanzo 4 : 11
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kutoka kwa mkono wako;
Ayubu 34 : 22
22 Hapana hofu ya giza kuu, mahali wawezapo kujificha watendao udhalimu.
Isaya 10 : 3
3 ⑫ Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?
Mathayo 23 : 33
33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya Jehanamu?
Warumi 2 : 3
3 Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?
1 Wathesalonike 5 : 3
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Waraka kwa Waebrania 2 : 3
3 sisi je! Tutapataje kupona, tukipuuza wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliomsikia;
Waraka kwa Waebrania 12 : 26
26 ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.
Leave a Reply