Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kutokuwa na Mungu
Kumbukumbu la Torati 7 : 10
10 naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake.
Kumbukumbu la Torati 32 : 15
15 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
1 Samweli 2 : 30
30 ⑬ Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nilisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau nitawadharau.
Ayubu 8 : 13
13 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;
Ayubu 35 : 10
10 Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku;
Zaburi 2 : 2
2 Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi[1] wake,
Zaburi 2 : 4
4 Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
Zaburi 9 : 17
17 Wadhalimu wataenda kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
Zaburi 10 : 4
4 Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Mungu Hatapatiliza. Mawazo yake yote ni, Hakuna Mungu;
Zaburi 14 : 3
3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
Zaburi 53 : 3
3 ⑲ Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
Warumi 3 : 11
11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
Warumi 3 : 18
18 Kumcha Mungu hakupo machoni pao.
Zaburi 28 : 5
5 Maana hawazifahamu kazi za BWANA, Wala matendo ya mikono yake, Atawavunja wala hatawajenga tena;
Isaya 5 : 12
12 ⑱ Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake.
Zaburi 36 : 1
1 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.
Zaburi 50 : 22
22 Yafahamuni hayo, Ninyi mnaomsahau Mungu, Nisije nikawararueni, Asipatikane wa kuwaokoa.
Zaburi 52 : 7
7 ⑭ Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.
Zaburi 53 : 4
4 ⑳ Je! Wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawakumwita MUNGU.
Zaburi 54 : 3
3 Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.
Zaburi 55 : 19
19 Mungu atawalaye tangu milele atanisikia; Na kuwaadhibu, maana hawajirekebishi, Wala kumcha Mungu.
Zaburi 86 : 14
14 Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Kundi la watu wakatili wanataka kuniua. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao.
Mithali 14 : 2
2 Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.
Isaya 1 : 3
3 Ng’ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.
Isaya 17 : 10
10 Maana umemsahau Mungu wa wokovu wako, wala hukuukumbuka mwamba wa ngome yako; kwa sababu hiyo ulipanda mashamba yapendezayo, na kutia ndani yake mizabibu migeni.
Isaya 22 : 11
11 Nanyi mlifanya birika la maji katikati ya kuta mbili, la kuwekea maji ya birika la kale; lakini hamkumwangalia yeye aliyeyafanya hayo, wala kumjali yeye aliyeyatengeneza zamani.
Isaya 30 : 2
2 waendao kuteremkia Misri wala hawakuuliza kinywani mwangu; ili wajitie nguvu kwa nguvu za Farao, na kutumainia kivuli cha Misri.
Isaya 30 : 13
13 basi, uovu huu utakuwa kwenu kama mahali palipobomoka, kuanguka patokezapo katika ukuta mrefu, ambapo kuvunjika kwake huja ghafla kwa mara moja.
Leave a Reply