Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kutoa hoja
Ayubu 13 : 3
3 Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi, Nami nataka kuhojiana na Mungu.
Ayubu 13 : 28
28 Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.
Kutoka 4 : 11
11 BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA?
Kutoka 20 : 5
5 ⑰ Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 : 11
11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Isaya 1 : 18
18 Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.
Isaya 5 : 4
4 Je! Ni kazi gani iliyohitajika kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibumwitu?
Isaya 43 : 26
26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.
Hosea 4 : 1
1 Lisikieni neno la BWANA, enyi wana wa Israeli; kwa maana BWANA ana shutuma nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.
Mika 6 : 2
2 ⑫ Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli.
Danieli 4 : 36
36 ④ Basi wakati huo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.
1 Wakorintho 10 : 15
15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.
1 Petro 3 : 15
15 Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa heshima.
Kumbukumbu la Torati 12 : 8
8 Msifanye kwa kufuata mambo yote tuyafanyayo hapa leo, kila mtu kama apendavyo;
Mithali 3 : 5
5 ③ Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Mithali 14 : 12
12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Luka 5 : 22
22 Na Yesu alijua hoja zao, akajibu akawaambia, Mnajiuliza nini mioyoni mwenu?
Luka 20 : 5
5 Wakaulizana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, Basi, mbona hamkumwamini?
Matendo 17 : 2
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimokuwa, akahojiana nao kwa maneno ya Maandiko sabato tatu,
Matendo 18 : 4
4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.
Matendo 24 : 25
25 Na Paulo alipokuwa akitoa hoja zake kuhusu haki, na kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja, Feliki akaingiwa na hofu na kusema, Sasa nenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.
Leave a Reply