Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuta za Miji
Kumbukumbu la Torati 3 : 6
6 Tukaiharibu kabisa, kama tulivyomfanya huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, kwa kuharibu kabisa kila mji uliokuwa na wanaume, wanawake na watoto.
Yoshua 2 : 15
15 Ndipo akawashusha kwa kamba dirishani, maana nyumba yake ilikuwa katika ukuta wa mji; naye alikaa ukutani.
Yeremia 51 : 44
44 Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.
Yeremia 51 : 58
58 BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
1 Samweli 31 : 10
10 Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa Maashtorethi; wakakitundika kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-sheani.
2 Samweli 11 : 20
20 kisha, ikiwa hasira ya mfalme itawaka, akakuambia, Kwa nini mliukaribia mji namna ile ili kuupiga? Je! Hamkujua ya kuwa watapiga mishale toka ukutani?
2 Samweli 20 : 15
15 ⑲ Na hao wakaja wakauzingira katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya kilima mbele ya mji, nacho kikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunjavunja ukuta, wapate kuubomoa.
2 Samweli 20 : 21
21 Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, jina lake, Sheba, mwana wa Bikri, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta.
Yoshua 2 : 15
15 Ndipo akawashusha kwa kamba dirishani, maana nyumba yake ilikuwa katika ukuta wa mji; naye alikaa ukutani.
2 Wafalme 25 : 4
4 ⑥ Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote;) mfalme akaenda kwa njia ya Araba.
Ufunuo 21 : 12
12 ⑪ ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya makabila kumi na mawili ya Waisraeli.
Ufunuo 21 : 14
14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi kulikuwa na majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-kondoo.
Ufunuo 21 : 21
21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
Leave a Reply