Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kusikiliza wengine
Yakobo 1 : 19
19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Mithali 12 : 15
15 ② Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
Mithali 19 : 27
27 ② Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.
Mithali 5 : 1 – 23
1 Mwanangu, sikiliza hekima yangu; Tega sikio lako, uzisikie akili zangu;
2 Upate kuilinda busara, Na midomo yako iyahifadhi maarifa.
3 Maana midomo ya malaya hudondosha asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili.
5 Miguu yake inateremkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutangatanga wala hana habari.
7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu.
8 Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9 Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakatili miaka yako;
10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;
11 Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho, Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
12 Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo, Na moyo wangu ukadharau kukemewa;
13 Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!
14 Nilikuwa karibu na kuingia katika maovu yote, Katikati ya mkutano na kusanyiko.
15 Unywe maji ya tangi lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako.
16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu?
17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe.
18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.
19 Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Matiti yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.
20 Mwanangu! Mbona unashangilia malaya, Na kukikumbatia kifua cha mgeni?
21 Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
22 Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.
23 Atakufa huyo kwa kukosa maonyo, Naye atapotea kwa wingi wa ujinga wake.
Mithali 18 : 13
13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
Mithali 11 : 14
14 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Mithali 21 : 23
23 Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.
Leave a Reply