Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kusikiliza muziki
Wakolosai 3 : 16
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Warumi 12 : 2
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Waefeso 5 : 19
19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
Wafilipi 4 : 8 – 12
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
9 Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
10 Nilifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.
11 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yoyote niliyo nayo.
12 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote, na katika mambo yoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
Warumi 10 : 17
17 Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Yohana 4 : 24
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Zaburi 118 : 19 – 29
19 ⑰ Nifungulieni malango ya haki, Nitaingia na kumshukuru BWANA.
20 ⑱ Lango hili ni la BWANA, Wenye haki ndio watakaoliingia.
21 Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu.
22 ⑲ Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni.⑳
23 Neno hili limetoka kwa BWANA, Nalo ni ajabu machoni petu.
24 Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia na kuifurahia.
25 Ee BWANA, utuokoe, twakusihi; Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.
26 Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA; Tumewabariki toka nyumbani mwa BWANA.
27 BWANA ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa kamba Pembeni mwa madhabahu.
28 Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.
29 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Waraka kwa Waebrania 2 : 12
12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
Zaburi 121 : 1 – 8
1 Nayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu hutoka kwa BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Hatauacha mguu wako usogezwe; Akulindaye hatasinzia;
4 Naam, hatasinzia wala hatalala, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
Yakobo 5 : 13
13 Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Yakobo 1 : 22
22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
1 Wakorintho 6 : 12
12 ⑬ Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote.
Leave a Reply