Biblia inasema nini kuhusu kushinda ulafi – Mistari yote ya Biblia kuhusu kushinda ulafi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kushinda ulafi

1 Wakorintho 9 : 24 – 27
24 ⑳ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo ili wapokee taji liharibikayo; bali sisi tupokee taji lisiloharibika.
26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiria wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Wafilipi 3 : 19
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao uko katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Mithali 23 : 21
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.

1 Petro 5 : 8
8 ⑲ Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Ayubu 23 : 10 – 12
10 Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
12 Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,

Warumi 8 : 5 – 8
5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
6 ⑲ Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
7 ⑳ Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

Warumi 14 : 17
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.

Warumi 6 : 12 – 13
12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.

Zaburi 131 : 2
2 ⑬ Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya Kifuani mwa mama yake; Roho yangu ni kama mtoto, Aliyeachishwa kunyonya.

Mithali 23 : 2
2 Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi.

Yohana 6 : 53
53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.

Yohana 6 : 48 – 51
48 ④ Mimi ndimi chakula cha uzima.
49 ⑤ Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa.
50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.
51 ⑥ Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

Mathayo 5 : 6
6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

1 Wakorintho 6 : 19 – 20
19 ⑲ Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 ⑳ maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *