Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kushinda roho
Mithali 11 : 30
30 Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu.
Mathayo 28 : 19
19 Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Danieli 12 : 3
3 Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.
Mathayo 10 : 32
32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Warumi 6 : 23
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
1 Wathesalonike 2 : 19 – 20
19 Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji la kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?
20 Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha yetu.
Wagalatia 6 : 7 – 8
7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Mathayo 11 : 28
28 Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Warumi 10 : 9
9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Yohana 15 : 16
16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Warumi 3 : 10
10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.
Luka 23 : 39 – 43
39 Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.
40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lolote lisilofaa.
42 ⑥ Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
Isaya 55 : 6
6 ⑲ Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yuko karibu;
Warumi 3 : 23
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Matendo 2 : 21
21 ② Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.
Warumi 10 : 13
13 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
Warumi 10 : 10
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Marko 16 : 15
15 ① Akawaambia, Nendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Yohana 3 : 5
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Ezekieli 33 : 1 – 9
1 Neno la BWANA likanijia, kusema,
2 ⑧ Mwanadamu, sema na wana wa watu wako, uwaambie, Hapo nitakapoleta upanga juu ya nchi, watu wa nchi hiyo wakimtwaa mtu mmoja miongoni mwao, na kumweka awe mlinzi wao;
3 akiona upanga unakuja juu ya nchi hiyo, na kupiga tarumbeta na kuwaonya watu;
4 ⑩ basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.
5 Aliisikia sauti ya tarumbeta, wala hakuonywa; damu yake itakuwa juu yake; lakini kama angalionywa, angalijiokoa roho yake.
6 ⑪ Bali mlinzi akiona upanga unakuja, kama hapigi tarumbeta, wala watu hawakuonywa, na upanga ukaja ukamwondoa mtu awaye yote miongoni mwao; ameondolewa huyo katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo.
7 ⑫ Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu.
8 ⑬ Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
9 ⑭ Lakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.
Leave a Reply