Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kusafisha
1 Mambo ya Nyakati 28 : 18
18 ⑬ na kwa madhabahu ya kufukizia, dhahabu iliyosafika sana kwa uzani; na dhahabu kwa mfano wa gari, yaani, makerubi, yenye kutandaza mabawa, na kulifunika sanduku la Agano la BWANA.
1 Mambo ya Nyakati 29 : 4
4 ⑳ yaani, talanta elfu tatu za dhahabu, za dhahabu ya Ofiri, na talanta elfu saba za fedha iliyosafika, ya kuzifunikiza kuta za nyumba;
Isaya 25 : 6
6 ⑲ Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
Isaya 1 : 25
25 nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote;
Isaya 48 : 10
10 ⑯ Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuri ya mateso.
Yeremia 9 : 7
7 ⑦ Basi, kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu; maana nisipotenda hivi, nitende nini kwa ajili ya binti ya watu wangu?
Zekaria 13 : 9
9 Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.
Malaki 3 : 3
3 naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea BWANA dhabihu katika haki.
Zaburi 18 : 30
30 Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya BWANA imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.
Zaburi 119 : 140
140 Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
Leave a Reply