Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kupoteza marafiki
Zaburi 34 : 17 โ 20
17 Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote.
18 BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na huwaokoa waliopondeka roho.
19 Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA kutoka kwayo yote.
20 โซ Huihifadhi mifupa yake yote, Usivunjike hata mmoja.
Mithali 18 : 24
24 Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
2 Wakorintho 12 : 9
9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Mithali 27 : 4 โ 6
4 Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
5 Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika.
6 Majeraha utiwazo na rafiki ni ya kweli; Bali busu la adui ni udanganyifu.
Wafilipi 4 : 19
19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Wakolosai 2 : 8
8 โฉ Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.
Yohana 15 : 18 โ 23
18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi niliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.
21 Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenituma.
22 Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana kisingizio kwa dhambi yao.
23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.
Leave a Reply