Biblia inasema nini kuhusu kupiga – Mistari yote ya Biblia kuhusu kupiga

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kupiga

Warumi 12 : 19
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

Kutoka 21 : 15
15 Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.

1 Yohana 4 : 8
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

Mambo ya Walawi 25 : 1 – 55
1 ③ Kisha BWANA akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia,
2 ④ Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya BWANA.
3 Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake;
4 lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa BWANA; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
5 ⑤ Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi.
6 Na hiyo Sabato ya nchi itakuwa chakula kwenu; kwako wewe, na kwa mtumishi wako, na kwa mjakazi wako, na kwa mtumishi aliyeajiriwa, na kwa mgeni wako akaaye pamoja nawe;
7 na kwa wanyama wako, na kwa wanyama walio katika nchi yako; mavuno yote yatakuwa ni chakula chao.
8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arubaini na tisa.
9 ⑥ Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.
10 ⑦ Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kuwatangazia uhuru watu wote katika nchi; itakuwa ni mwaka wa jubilii[13] kwenu; na kila mtu atairudia milki yake, na kila mtu atarejea kwa jamaa yake.
11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni jubilii kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
12 Kwa kuwa ni jubilii; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula mavuno yake yatokayo shambani.
13 ⑧ Mwaka huo wa jubilii mtairudia kila mtu milki yake.
14 ⑩ Tena kama ukimwuzia jirani yako chochote, au kununua chochote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe;
15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya jubilii, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe.
16 Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo.
17 ⑪ Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
18 ⑫ Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama.
19 Nayo nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba, na kuishi humo salama.
20 ⑬ Na kama mkisema, Je! Mwaka wa saba tutakula nini? Angalieni hatutapanda mbegu, wala kukusanya mavuno yetu;
21 ⑭ ndipo nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita, nayo inchi itazaa matunda ya kutosha miaka mitatu.
22 ⑮ Na mwaka wa nane mtapanda mbegu, na kuyala yale matunda, akiba hiyo ya zamani, hata mwaka wa tisa, hadi matunda yake yatakapoletwa ndani, mtakula hiyo akiba ya zamani.
23 ⑯ Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wapangaji wangu.
24 Nanyi mtatoa ukombozi kwa ajili ya nchi, katika eneo lote la milki yenu.
25 ⑰ Ikiwa nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye.
26 Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa;
27 ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake.
28 Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hadi mwaka wa jubilii; na katika jubilii ataliachilia, naye mwenyewe atairejea milki yake.
29 Tena ikiwa mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo ndani ya mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima baada ya kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima.
30 Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika jubilii.
31 Lakini nyumba za vijiji, ambavyo havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya nchi; nazo zina ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika jubilii.
32 ⑱ Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yoyote.
33 Tena mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa nyumba iliyouzwa na mji wa milki yake, itatoka katika jubilii; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli.
34 ⑲ Lakini konde la malisho ya miji yao lisiuzwe kwa kuwa ni milki yao ya daima.
35 ⑳ Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri.
36 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe.
37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.
38 Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu.
39 Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimfanye akutumikie kama mtumwa;
40 kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hadi mwaka wa jubilii;
41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake.
42 Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe kama watumwa.
43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako.
44 Tena kuhusu watumishi wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando yenu, katika hao mtanunua watumishi na wajakazi.
45 Tena wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu.
46 Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumishi wenu kwa hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli.
47 Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni;
48 baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa;
49 au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu yeyote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kama yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe.
50 Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa jubilii; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo.
51 Ikiwa ingali imesalia miaka mingi, kama hesabu yake ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo alinunuliwa kwayo.
52 Tena kama imesalia miaka michache tu hadi mwaka wa jubilii, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake.
53 Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hadi mwaka, ndivyo atakavyokuwa pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako.
54 Tena kwamba hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, ndipo atatoka katika mwaka wa jubilii, yeye, pamoja na watoto wake.
55 Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Kumbukumbu la Torati 22 : 6 – 7
6 ⑱ Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wowote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda;
7 ⑲ sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi.

Kutoka 23 : 10 – 11
10 Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kupata mavuno yake;
11 lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo hivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni.

Yohana 18 : 1 – 40
1 ④ Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng’ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake.
2 ⑤ Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake. ⑥
3 Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
4 ⑦ Basi Yesu, huku akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta?
5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
6 Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini.
7 Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.
8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.
9 ⑧ Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao.
10 Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kulia. Na yule mtumwa jina lake ni Malko.
11 ⑩ Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?
12 ⑪ Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga.
13 Wakampeleka kwa Anasi kwanza; maana alikuwa baba mkwe wa Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule.
14 ⑫ Naye Kayafa ndiye yule aliyewapa Wayahudi lile shauri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
15 ⑬ Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika ukumbi wa Kuhani Mkuu.
16 Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mlinda mlango, akamleta Petro ndani.
17 Basi yule kijakazi, aliyekuwa mlinda mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi.
18 Na wale watumwa na watumishi walikuwa wakisimama, wamewasha moto wa makaa; maana kulikuwa na baridi; wakawa wakiota moto. Petro naye alikuwapo pamoja nao, anaota moto.
19 Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu kuhusu wanafunzi wake, na kuhusu mafundisho yake.
20 ⑭ Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.
21 Ya nini kuniuliza mimi? Waulize wale waliosikia ni nini niliyowaambia; wao wanajua niliyoyanena.
22 ⑮ Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?
23 Yesu akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini?
24 Basi Anasi akampeleka akiwa amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu.
25 Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi.
26 Mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu, naye ni jamaa yake yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Je! Mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?
27 Basi Petro akakana tena, na mara jogoo akawika.
28 ⑯ Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio,[5] nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka.
29 Basi Pilato akawatokea nje, akasema, Ni mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu?
30 Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako.
31 ⑰ Basi Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu.
32 ⑱ Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionesha ni mauti gani atakayokufa.
33 Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
34 ⑲ Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?
35 ⑳ Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.
37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
38 Pilato akamwambia, Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yoyote kwake.
39 Lakini kwenu kuna desturi ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka; basi, mwapenda niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?
40 Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang’anyi.

Yuda 1 : 7
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *