Biblia inasema nini kuhusu Kupiga – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kupiga

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kupiga

Kutoka 5 : 14
14 ⑧ Na wanyapara wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?

Kumbukumbu la Torati 25 : 3
3 ⑱ Aweza kumpiga fimbo arubaini asizidishe asije akaonekana nduguyo kuwa amedharauliwa kwako, azidishapo kwa kumpiga fimbo nyingi juu ya hizi.

Marko 13 : 9
9 Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.

Matendo 5 : 40
40 Wakakubali maneno yake; nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao.

Matendo 16 : 22
22 Makutano wote wakaondoka wakawaendea, mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.

Matendo 16 : 37
37 ② Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe.

Matendo 18 : 17
17 Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu.

Matendo 21 : 32
32 Mara akatwaa askari na maofisa, akawaendea mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *