Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kupata pamoja na wengine
1 Yohana 4 : 19 โ 21
19 Sisi tunapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.
20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Warumi 12 : 18
18 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
Yohana 13 : 34
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Waraka kwa Waebrania 12 : 14
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Mithali 19 : 11
11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Mithali 17 : 14
14 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
Yohana 11 : 35
35 Yesu akalia machozi.
Mathayo 6 : 12 โ 15
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
1 Petro 5 : 3 โ 5
3 โญ Wala si kama wajifanyao mabwana wa wale walio chini ya utunzaji wao, bali iweni mifano kwa lile kundi.
4 โฎ Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtalipokea taji la utukufu, lile lisilokauka.
5 โฏ Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
Zaburi 133 : 1 โ 3
1 Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.
2 Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
3 Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
Mithali 12 : 16
16 Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.
Mithali 27 : 6
6 Majeraha utiwazo na rafiki ni ya kweli; Bali busu la adui ni udanganyifu.
Leave a Reply