Biblia inasema nini kuhusu kuongezewa damu – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuongezewa damu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuongezewa damu

Matendo 15 : 29
29 yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.

Yohana 15 : 13
13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

Mambo ya Walawi 17 : 14
14 Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe uko katika damu yake; ndio nikawaagiza wana wa Israeli, Msiile damu ya mnyama wa aina yoyote; kwa kuwa uhai wa kila kiumbe ni damu yake; yeyote atakayeila atatengwa.

Yohana 6 : 53 – 57
53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 ⑧ Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.

Mathayo 24 : 34
34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.

Mambo ya Walawi 3 : 17
17 Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.

Mwanzo 9 : 4
4 Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.

Mambo ya Walawi 17 : 13
13 Mtu yeyote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunikia mchangani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *