Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuongeza kwenye biblia
Ufunuo 22 : 18 – 19
18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
19 Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
Kumbukumbu la Torati 4 : 2
2 ⑤ Msiliongeze neno ninalowaamuru wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, ninazowaamuru.
Mithali 30 : 5 – 6
5 ⑲ Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
6 ⑳ Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
Ufunuo 22 : 18
18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Ufunuo 22 : 19
19 Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
Kumbukumbu la Torati 12 : 32
32 ⑯ Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze.
Leave a Reply