Biblia inasema nini kuhusu Kunguru – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kunguru

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kunguru

Mithali 30 : 17
17 Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila.

Wimbo ulio Bora 5 : 11
11 Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana, Nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru;

Mambo ya Walawi 11 : 15
15 na kila kunguru kwa aina zake;

Kumbukumbu la Torati 14 : 14
14 na kila kunguru kwa aina zake;

Mwanzo 8 : 7
7 akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huku na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.

1 Wafalme 17 : 6
6 Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.

Luka 12 : 24
24 ① Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *