Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kumngoja Mungu
Yeremia 14 : 22
22 ② Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.
Zaburi 25 : 5
5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.
Zaburi 104 : 28
28 Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema;
Zaburi 145 : 16
16 Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
Zaburi 123 : 2
2 Kama vile macho ya watumishi Yanavyoutegemea mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Yanavyoutegemea mkono wa bimkubwa wake; Ndivyo macho yetu yanavyomtegemea BWANA, Mungu wetu, Hadi atakapoturehemu.
Zaburi 39 : 8
8 Uniokoe kutoka kwa maasi yangu yote, Usinifanye niwe wa kulaumiwa na mpumbavu.
Luka 2 : 25
25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
Mwanzo 49 : 18
18 Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.
Zaburi 62 : 2
2 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika.
Zaburi 25 : 5
5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.
Zaburi 33 : 20
20 Nafsi zetu zinamngoja BWANA; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Zaburi 59 : 10
10 Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kutazama kwa ushindi juu ya adui zangu.
Habakuki 2 : 3
3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Matendo 1 : 4
4 Wakati alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kutoka kwangu;
Wagalatia 5 : 5
5 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.
1 Wakorintho 1 : 7
7 hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;
Leave a Reply