Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kumkimbia Mungu
2 Petro 3 : 9
9 โฏ Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.
Zaburi 139 : 7 โ 10
7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 โณ Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kulia utanishika.
Yona 2 : 1 โ 10
1 Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, akiwa katika tumbo la yule samaki,
2 Akasema, Nilimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu niliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.
3 Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu;
6 Nilishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni, Ee BWANA, Mungu wangu,
7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nilimkumbuka BWANA; Maombi yangu yakakufikia, Katika hekalu lako takatifu.
8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo Hujitenga na rehema zao wenyewe.
9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA.
10 BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.
Yeremia 17 : 9
9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Mathayo 12 : 40
40 Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.
Leave a Reply