Biblia inasema nini kuhusu kumchukia ndugu yako – Mistari yote ya Biblia kuhusu kumchukia ndugu yako

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kumchukia ndugu yako

1 Yohana 3 : 15
15 ⑱ Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukaao ndani yake.

Warumi 12 : 19
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

Luka 10 : 27
27 ① Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

Luka 14 : 26
26 ⑥ Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. ⑦

1 Timotheo 5 : 8
8 Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *