Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kulinda israel
Zaburi 122 : 6
6 Uombeeni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao;
Zekaria 12 : 1 – 14
1 Ufunuo wa neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.
2 Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbayumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.
3 Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata majeraha mengi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.
4 Katika siku hiyo, asema BWANA, nitamtia kila farasi ushangao, na yeye ampandaye nitamtia wazimu; nami nitaifunulia nyumba ya Yuda macho yangu, nami nitamtia upofu kila farasi wa hayo makabila ya watu.
5 Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu wana nguvu katika BWANA wa majeshi, Mungu wao.
6 Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kulia na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusalemu.
7 Naye BWANA ataziokoa hema za Yuda kwanza, ili utukufu wa nyumba ya Daudi, na utukufu wa wenyeji wa Yerusalemu, usipate kutukuzwa kuliko Yuda.
8 Katika siku hiyo BWANA atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa BWANA mbele yao.
9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitayaangamiza mataifa yote yatakayokuja kupigana na Yerusalemu.
10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimdunga; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao.
Mwanzo 12 : 3
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Isaya 60 : 12
12 Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa.
Hesabu 24 : 9
9 ⑱ Aliinama, akalala mfano wa simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha? Na abarikiwe kila akubarikiye, Na alaaniwe kila akulaaniye.
Zaburi 83 : 1 – 18
1 Ee Mungu, usistarehe, Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.
2 ⑧ Maana adui zako wanafanya ghasia, Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao.
3 ⑩ Juu ya watu wako wanafanya hila, Na kushauriana juu yao uliowaficha.
4 ⑪ Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.
5 Maana wanashauriana kwa moyo mmoja, Juu yako wanafanyana agano.
6 Hema za Edomu, na Waishmaeli, Na Moabu, na Wahagari,
7 Gebali, na Amoni, na Amaleki, Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,
8 Ashuri naye amepatana nao, Wamewasaidia wana wa Lutu.
9 ⑫ Uwatende kama ulivyowatenda Midiani, Sisera, Na Yabini, penye kijito cha Kishoni.
10 Ambao waliangamizwa Endori; Wakawa samadi juu ya nchi.
11 ⑬ Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, Na wakuu wao wote kama Zeba na Zalmuna.
12 Ambao Walisema, Na tutamalaki makao ya Mungu.
13 Ee Mungu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, Kama ya makapi mbele ya upepo,
14 Kama moto uteketezao msitu, Kama miali ya moto iiwashayo milima,
15 Ndivyo utakavyowafuatia kwa tufani yako, Na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16 Uzijaze nyuso zao fedheha; Ili wapate kulitafuta jina lako, Ee BWANA.
17 Waaibike, wafadhaike milele, Naam, watahayarike na kupotea.
18 Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.
Zekaria 2 : 8
8 Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.
Yoeli 3 : 1 – 3
1 Kwa maana,[2] angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu,
2 ⑱ nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, na kwa ajili ya urithi wangu, Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.
3 ⑲ Nao wamewapigia kura watu wangu; na mvulana wamemwuza ili kupata kahaba, na msichana wamemwuza ili kupata divai, wapate kunywa.
Isaya 41 : 11 – 12
11 ③ Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.
12 Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.
Yoeli 3 : 1
1 Kwa maana,[2] angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu,
Malaki 3 : 6
6 Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
Warumi 11 : 1 – 36
1 Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? La hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazawa wa Abrahamu, mtu wa kabila la Benyamini.
2 Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na Maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,
3 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimebaki peke yangu, nao wananitafuta roho yangu.
4 ① Lakini lile jibu la Mungu lamwambiaje? Nimejibakizia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali.
5 ② Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.
6 ③ Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema.
7 ④ Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu.
8 ⑤ Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo.
9 ⑥ Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;
10 Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote.
11 ⑦ Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? La hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikia Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.
12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?
13 Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu,
14 ⑧ nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao.
15 Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
16 ⑩ Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika.
17 ⑪ Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
18 ⑫ usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.
19 Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.
20 ⑬ Vema. Yalikatwa kwa kutoamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.
22 ⑭ Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.
23 ⑮ Na hao pia, wasipokaa katika kutoamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena.
24 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe?
25 ⑯ Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 ⑰ Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 ⑱ Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.
28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
29 Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.
30 Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao;
31 kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema.
32 ⑲ Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
33 ⑳ Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!
34 Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?
35 Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena?
36 Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.
Kumbukumbu la Torati 28 : 1 – 68
1 ⑳ Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, kuongezeka kwa ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
7 BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
8 BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
9 BWANA atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya BWANA, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.
10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.
11 BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
12 Atakufunulia BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.
13 BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;
14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lolote, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, kuongezeka kwa ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.
19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,
20 BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.
21 BWANA atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.
22 BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa joto jingi, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.
24 BWANA atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
25 BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huku na huko katika falme zote za duniani.
26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
27 BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
28 BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
29 utakwenda kwa kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.
31 Ng’ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang’anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo wako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.
32 Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.
33 Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima;
34 hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona.
35 BWANA atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.
36 BWANA atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe.
37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.
38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.
39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu.
40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.
41 Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.
42 Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo.
43 Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.
44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.
45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;
46 nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele;
47 ① kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;
48 ② kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
49 ③ BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;
50 ④ taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;
51 ⑤ naye atakula uzao wa ng’ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala kuongezeka kwa ng’ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
52 ⑥ Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa BWANA, Mungu wako.
53 ⑦ Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa BWANA, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
54 Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu ya masalio ya wanawe waliosalia naye;
55 hata asitake wao mmojawapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilichomsalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote.
56 Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatarisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake,
57 ⑧ na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako.
58 ⑩ Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;
59 ⑪ ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.
60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.
61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha Torati hii, atakutia nayo BWANA juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa.
62 ⑫ Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako.
63 ⑬ Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi BWANA juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi BWANA juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.
64 ⑭ BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe.
65 ⑮ Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini BWANA atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika;
66 na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako;
67 ⑯ asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.
68 ⑰ BWANA atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena popote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.
2 Mambo ya Nyakati 17 : 10
10 ⑪ Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati.
Nehemia 4 : 17 – 18
17 Watu wale walioujenga ukuta, na wale waliochukua mizigo, walijitweka wenyewe, kila mtu alifanya kazi kwa mkono mmoja, na kwa mkono wake wa pili alishika silaha yake;
18 nao wajenzi, kila mtu alikuwa na upanga wake, umefungwa ubavuni mwake, ndivyo alivyojenga. Na yeye aliyepiga baragumu alikuwa karibu na mimi.
Kumbukumbu la Torati 28 : 47 – 48
47 ① kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;
48 ② kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
Hesabu 31 : 3
3 Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipizia kisasi BWANA, juu ya Midiani.
Ezekieli 39 : 1 – 29
1 Na wewe, mwanadamu, tabiri juu ya Gogu, useme, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali;
2 nami nitakugeuza na kukuongoza, nami nitakupandisha toka pande za mwisho za kaskazini; nami nitakuleta juu ya milima ya Israeli;
3 nami nitaupiga upinde wako, utoke katika mkono wako wa kushoto, na mishale yako nitaiangusha, itoke katika mkono wako wa kulia.
4 Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa pori, uliwe na wao.
5 Utaanguka katika uwanda; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.
6 Nami nitapeleka moto juu ya Magogu; na juu ya watu wote wakaao salama katika visiwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
7 Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulikana kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, na Aliye Mtakatifu katika Israeli.
8 Tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema Bwana MUNGU; hii ndiyo siku ile niliyoinena.
9 Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba;
10 hata hawataokota kuni mashambani, wala hawatakata kuni msituni; maana watafanya mioto kwa silaha zile; nao watawateka nyara watu waliowateka wao, na kuwapora watu waliowapora wao, asema Bwana MUNGU.
11 Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na jamii ya watu wake wote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
12 Na kwa muda wa miezi saba, nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuitakasa nchi.
13 Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU.
14 Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watachunguza.
15 Na hao wapitao kati ya nchi watachunguza; na mtu yeyote aonapo mfupa wa mtu, ndipo atakapoweka alama karibu nao, hadi wazikaji watakapouzika katika bonde la Hamon-Gogu.
16 Tena, Hamona litakuwa jina la mji. Hivyo ndivyo watakavyotakasa nchi.
17 Na wewe, mwanadamu, Bwana MUNGU asema hivi; Sema na ndege wa kila namna, na kila mnyama wa porini, Jikusanyeni, mje; jikusanyeni pande zote mwijie karamu yangu ya kafara ninayoandaa kwa ajili yenu, naam, karamu kuu ya kafara juu ya milima ya Israeli, mpate kula nyama na kunywa damu.
18 Mtakula nyama yao walio hodari, na kunywa damu ya wakuu wa dunia, ya kondoo dume na ya wana-kondoo, na ya mbuzi, na ya ng’ombe, wote na wanono wa Bashani.
19 Nanyi mtakula mafuta na kushiba, mtakunywa damu na kulewa, katika karamu yangu ya kafara ninayoiandaa kwa ajili yenu.
20 Nanyi mtashibishwa mezani pangu kwa farasi, na magari ya vita, na mashujaa, na watu wote wa vita, asema Bwana MUNGU.
21 ① Nami nitauweka utukufu wangu kati ya mataifa, na mataifa wote wataiona hukumu yangu niliyoitekeleza, na mkono wangu niliouweka juu yao.
22 Basi, nyumba ya Israeli watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, tangu siku hiyo na baadaye.
23 ② Nao mataifa watajua ya kuwa nyumba ya Israeli walihamishwa, na kwenda kifungoni, kwa sababu ya uovu wao; kwa sababu waliniasi, nami nikawaficha uso wangu; basi nikawatia katika mikono ya adui zao, nao wote wakaanguka kwa upanga pia.
24 ③ Kwa kadiri ya uchafu wao, kwa kadiri ya makosa yao, ndivyo nilivyowatenda, nami nikawaficha uso wangu.
25 ④ Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Sasa nitawarejesha watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu takatifu.
26 ⑤ Nao watachukua aibu yao, na makosa yao yote waliyoniasi, watakapokaa salama katika nchi yao wenyewe, wala hapana mtu atakayewatia hofu;
27 ⑥ nitakapokuwa nimewaleta tena kutoka makabila ya watu, na kuwakusanya kwa kuwatoa katika nchi za adui zao, na kutakaswa kati yao mbele ya macho ya mataifa mengi.
28 ⑦ Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, kwa kuwa niliwahamisha, waende utumwani kati ya mataifa, na mimi nikawakusanya, na kuwaingiza katika nchi yao wenyewe; wala sitawaacha tena huko kamwe, hata mmojawapo;
29 ⑧ wala sitawaficha uso wangu tena; kwa maana nimemwaga roho yangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.
Kumbukumbu la Torati 32 : 9 – 10
9 Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.
10 Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho;
Leave a Reply