Biblia inasema nini kuhusu kulala – Mistari yote ya Biblia kuhusu kulala

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kulala

Mithali 3 : 24
24 ⑱ Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.

Zaburi 4 : 8
8 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Zaburi 127 : 2
2 Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.

Mithali 20 : 13
13 ⑩ Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.

Zaburi 132 : 4 – 5
4 ⑭ Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia;
5 Hadi nitakapompatia BWANA mahali, Na Mwenye nguvu wa Yakobo maskani”.

Mithali 6 : 10
10 ① Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!

Mithali 6 : 9
9 Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

Yohana 11 : 12
12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona.

Mathayo 9 : 24
24 akawaambia, Ondokeni; kwa maana msichana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.

Mathayo 8 : 24
24 Kukawa na msukosuko mkuu baharini, hata mashua ikafunikwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.

1 Wathesalonike 4 : 15 – 16
15 Kwa kuwa tunawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *