Biblia inasema nini kuhusu kulainisha moyo โ€“ Mistari yote ya Biblia kuhusu kulainisha moyo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kulainisha moyo

Ezekieli 36 : 26
26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.

Ezekieli 11 : 19
19 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;

Yeremia 17 : 9
9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Yohana 12 : 39 โ€“ 40
39 โ‘ซ Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,
40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

Mwanzo 6 : 5
5 BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote.

Matendo 16 : 31
31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.

Mathayo 15 : 19
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

Mwanzo 20 : 6
6 Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.

Kutoka 9 : 16
16 lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuoneshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.

Yeremia 24 : 7
7 Nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni BWANA; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *