Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kukemea
Mathayo 18 : 15 – 17
15 ④ Na ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
16 ⑤ La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
17 ⑥ Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Mithali 27 : 5
5 Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika.
1 Timotheo 5 : 20
20 Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
2 Timotheo 3 : 16 – 17
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
2 Timotheo 4 : 2
2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
Wagalatia 6 : 1
1 ⑳ Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Tito 2 : 15
15 Nena mambo hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
Waraka kwa Waebrania 4 : 12
12 ⑳ Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Mithali 1 : 23
23 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.
1 Timotheo 5 : 1
1 Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na wanaume vijana kama ndugu;
Mithali 29 : 15
15 Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
Mithali 27 : 6
6 Majeraha utiwazo na rafiki ni ya kweli; Bali busu la adui ni udanganyifu.
Yakobo 5 : 20
20 ④ jueni ya kuwa yeye amrejeshaye mwenye dhambi hadi akatoka katika njia ya upotevu, ataokoa roho ya mwenye dhambi kutoka mauti, na kufunika wingi wa dhambi.
Leave a Reply