Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kukata tamaa
Hesabu 17 : 13
13 Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya BWANA, hufa; je! Tutakufa sote pia?
Kumbukumbu la Torati 28 : 67
67 โฏ asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.
Ayubu 3 : 26
26 Mimi sioni raha, wala situlii, wala kupumzika; Lakini taabu huja.
Ayubu 17 : 16
16 Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini.
Zaburi 31 : 22
22 Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.
Zaburi 77 : 9
9 โฐ Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?
Mithali 13 : 12
12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.
Isaya 2 : 19
19 โ Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
Yeremia 2 : 25
25 Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu; lakini wewe ulisema, Hakuna matumaini kabisa; la, maana nimewapenda wageni, nami nitawafuata.
Yeremia 8 : 20
20 Mavuno yamepita, wakati wa joto umekwisha, wala sisi hatukuokoka.
Yeremia 18 : 12
12 Lakini wao wasema, Hakuna tumaini lolote; maana sisi tutafuata mawazo yetu wenyewe, nasi tutatenda kila mmoja wetu kwa kuufuata ushupavu wa moyo wake mbaya.
Maombolezo 3 : 21
21 Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini.
Maombolezo 5 : 22
22 Ingawa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.
Hosea 10 : 8
8 Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.
Yona 2 : 4
4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
Mika 7 : 7
7 Lakini mimi, nitamtazamia BWANA; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.
Mathayo 24 : 30
30 โ ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
Luka 13 : 28
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Abrahamu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
Luka 23 : 30
30 Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tufunikeni.
Ufunuo 6 : 17
17 โฑ Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kuistahimili?
Leave a Reply