Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kujiuzulu
Ayubu 5 : 17
17 ⑪ Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.
Ayubu 34 : 31
31 Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu, Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa;
Zaburi 4 : 4
4 Muwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
Zaburi 46 : 10
10 ⑰ Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
Mithali 3 : 11
11 ⑧ Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.
Mithali 18 : 14
14 Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?
Yeremia 51 : 50
50 Ninyi mliojiepusha na upanga, Nendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni BWANA tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
Maombolezo 3 : 39
39 Mbona anung’unika mwanadamu aliye hai Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?
Mika 6 : 9
9 Sauti ya BWANA inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.
Mathayo 6 : 10
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Luka 11 : 2
2 ⑦ Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]
Luka 21 : 19
19 Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.
Warumi 12 : 12
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;
Wafilipi 2 : 14
14 ① Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,
Wafilipi 4 : 13
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Wakolosai 1 : 11
11 mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
1 Wathesalonike 3 : 3
3 mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa ndizo tulizowekewa.
2 Timotheo 2 : 3
3 Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
2 Timotheo 4 : 5
5 Bali wewe, uwe mwenye kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza huduma yako kwa ukamilifu.
Waraka kwa Waebrania 10 : 34
34 Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
Waraka kwa Waebrania 12 : 12
12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
Yakobo 1 : 10
10 bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana atatoweka kama ua la majani.
Yakobo 4 : 7
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Yakobo 5 : 13
13 Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
1 Petro 1 : 6
6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa muda mfupi, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
1 Petro 4 : 13
13 ⑤ Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili pia katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.
1 Petro 4 : 19
19 ⑪ Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.
Leave a Reply