Biblia inasema nini kuhusu kujiepusha na nyama – Mistari yote ya Biblia kuhusu kujiepusha na nyama

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kujiepusha na nyama

Matendo 15 : 29
29 yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.

Mambo ya Walawi 11 : 1 – 47
1 BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
2 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi.
3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu iliyopasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.
4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
6 ① Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
7 ② Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
8 ③ Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
9 ④ Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.
10 ⑤ Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu,
11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu.
12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.
13 ⑥ Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu;
14 na mwewe, na kozi kwa aina zake,
15 na kila kunguru kwa aina zake;
16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;
17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa;
18 ⑦ na mumbi, na mwari, na mderi;
19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo.
20 Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu.
21 Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi;
22 ⑧ katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake.
23 Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu.
24 Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
25 ⑩ na mtu awaye yote atakayechukua chochote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni.
26 Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi.
27 Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.
28 Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu.
29 ⑪ Miongoni mwa viumbe watambaao juu ya nchi, hawa ni najisi kwenu; kicheche, panya na mjombakaka kwa aina zake,
30 ⑫ na guruguru kenge, mjusi, goromoe na lumbwi.
31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; yeyote atakayewagusa, wakiisha kuwa mgoza, atakuwa ni najisi hata jioni.
32 ⑬ Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi.
33 ⑭ Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa.
34 Chakula chochote cha kuliwa kitakuwa najisi kikitiwa maji ya chombo hicho; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi.
35 Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande chochote cha mizoga yao kitakuwa najisi; iwe ni tanuri, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu.
36 Pamoja na hayo, chemchemi, au shimo, ambamo maji yakusanyika, vitakuwa ni safi; lakini hicho kitakachogusa mizoga yao kitakuwa ni najisi.
37 Na kipande chochote cha mzoga kikiwa kimeangukia mbegu za kupandwa, zitakazopandwa zitakuwa safi.
38 Lakini ikiwa hizo mbegu zilitiwa maji na chochote cha mizoga yao kuziangukia, ni najisi kwenu.
39 Mnyama yeyote ambaye mna ruhusa kumla akifa, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hadi jioni.
40 ⑮ Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hadi jioni.
41 Na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa.
42 Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo.
43 ⑯ Msifanye nafsi zenu kuwa ni chukizo kwa kitu chochote chenye kutambaa, kitambaacho, wala msifanye nafsi zenu kuwa ni najisi kwa vitu hivyo, mkajipatia uchafu kwa hivyo.
44 ⑰ Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya nchi.
45 ⑱ Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.
46 Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi;
47 ⑲ ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.

1 Timotheo 4 : 3
3 ⑬ wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

1 Timotheo 4 : 1 – 16
1 ⑫ Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
3 ⑬ wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
4 ⑭ Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;
5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
6 Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoefu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.
7 ⑮ Bali hadithi za kale, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.
8 ⑯ Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
9 ⑰ Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa;
10 ⑱ kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa wale waaminio.
11 Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.
12 ⑲ Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma Maandiko, kuonya na kufundisha.
14 ⑳ Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
15 Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.
16 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako, na wale wakusikiao pia.

Isaya 65 : 25
25 Mbwamwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema BWANA.

Warumi 14 : 21
21 Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *