Biblia inasema nini kuhusu Kujibanza – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kujibanza

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kujibanza

Ayubu 31 : 1
1 Nilifanya agano na macho yangu; Basi ningewezaje kumwangalia msichana?

Mathayo 5 : 28
28 ⑯ lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Mathayo 19 : 12
12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Warumi 13 : 13
13 ⑧ Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.

1 Wakorintho 7 : 9
9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.

1 Wakorintho 7 : 29
29 Lakini, ndugu, nasema hivi, muda ubakio si mwingi; basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;

1 Wakorintho 7 : 38
38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.

1 Wakorintho 9 : 27
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiria wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Wakolosai 3 : 5
5 Basi, viueni viungo vyenu vilivyo vya kidunia, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;

1 Timotheo 4 : 12
12 ⑲ Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

1 Timotheo 5 : 2
2 wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.

Ufunuo 14 : 1
1 ⑮ Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu elfu mia moja na arubaini na nne pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.

Mwanzo 39 : 12
12 ② huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.

2 Samweli 11 : 13
13 Naye Daudi akamwalika, akala, akanywa mbele yake; naye akamlevya; hadi wakati wa jioni akatoka kwenda kulala kitandani mwake pamoja na watumishi wa bwana wake, lakini hakushuka nyumbani kwake.

Ruthu 3 : 13
13 ⑦ Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; BWANA aishivyo. Ulale wewe hadi asubuhi.

Mathayo 1 : 25
25 asimjue kamwe hadi alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.

1 Wakorintho 7 : 8
8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *