Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuiombea serikali
1 Timotheo 2 : 1 โ 4
1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
Warumi 13 : 1
1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Yeremia 29 : 7
7 โข Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa BWANA; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani.
1 Petro 2 : 17
17 โฎ Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.
1 Timotheo 2 : 1 โ 15
1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
6 ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.
7 Nami kwa ajili ya huo niliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.
8 Basi, nataka wanaume waombe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.
9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe msikivu.
13 โ Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
14 โก Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
15 Lakini ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
2 Mambo ya Nyakati 7 : 14
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Zaburi 22 : 28
28 โฒ Maana ufalme ni wa BWANA, Naye ndiye awatawalaye mataifa.
Mithali 11 : 14
14 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Danieli 2 : 20 โ 23
20 Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake.
21 Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;
22 yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.
23 Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme.
Mika 2 : 13
13 Avunjaye amekwea juu mbele yao; Wamebomoa mahali, wakapita mpaka langoni, Wakatoka nje huko; Mfalme wao naye amepita akiwatangulia, Naye BWANA ametangulia mbele yao.
Zaburi 2 : 10 โ 12
10 Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima, Enyi watawala wa dunia, mwaonywa.
11 Mtumikieni BWANA kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.
12 Shikeni yaliyo bora,[2] asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Ayubu 12 : 23 โ 25
23 Huyaongeza mataifa, na kuyaangamiza; Huyaeneza mataifa mbali, na kuyaacha.
24 Huwaondolea moyo wakuu wa watu wa nchi, Na kuwapoteza nyikani pasipokuwa na njia.
25 Wao hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga, Naye huwafanya kupepesuka kama mlevi.
2 Wakorintho 4 : 4
4 โฒ ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Danieli 9 : 18 โ 19
18 Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.
19 Ee Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.
1 Timotheo 2 : 1 โ 2
1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
Mathayo 12 : 25
25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yoyote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.
Mithali 28 : 2
2 Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa
Yeremia 17 : 7 โ 8
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa joto ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.
Zaburi 2 : 1 โ 4
1 Mbona mataifa yanafanya ghasia, Na watu kuwaza mambo ya bure?
2 Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi[1] wake,
3 Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupa mbali nasi kamba zao.
4 Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
Leave a Reply